Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Featured post

Behind the Scenes: Nilipobeba Red Raven na Crane 3 – Kazi ya Kisanaa Iliyojaa Moto

  Kuna wakati unapopiga picha ya kawaida. Kisha kuna wakati unaposhika silaha zako, ukiwa tayari kutengeneza kazi ya kisanaa itakayobeba hisia, uzito, na ubunifu wa kiwango cha juu. Katika picha hii ya behind the scenes, nilikuwa kwenye location, nikiwa nimeshika kamera ya RED Raven kwa mkono mmoja na gimbal ya Crane 3 kwa mkono mwingine — tayari kuunda magic nyuma ya lens. RED Raven si kamera ya kawaida. Ni silaha ya kweli kwa mtu anayejua thamani ya rangi, mwanga, na storytelling. Kamera hii inatumiwa na watayarishaji wa sinema kubwa duniani kwa sababu ina uwezo wa kunasa undani wa kila fremu kwa ubora wa sinema ya kweli. Ukiwa nayo mikononi, unajisikia kuwa sehemu ya kitu kikubwa zaidi ya wewe mwenyewe. Gimbal ya Crane 3 nayo ni kifaa kisichoweza kupuuzwa. Ili kuhakikisha kila mwendo wa kamera unakuwa laini, wenye utulivu na mvuto wa sinema, nilitegemea gimbal hii kama dereva tegemezi wa ubunifu wangu. Nilipokuwa kwenye shoot, niliweza kusogea mbele na nyuma, kupaa juu ya vi...

Cinematic vlog

 


SIKU YA KWANZA – MUGA AMEFIKA NAIROBI (VALENTINE)

Siku ya Valentine, wakati watu wanapokea maua, chocolate na “I love you”, Muga alikuwa anashuka kwa basi pale Machakos terminal, akiwa na begi moja la nguo, simu yenye betri ya 18%, na mfuko wenye mia chache.

Nairobi ilimkaribisha kwa kelele, baridi na haraka zake. Hakuna aliyemjua. Hakuna aliyemsubiri.

Alitembea mpaka Eastleigh, akipata chumba kidogo cha kulala kwa siku moja. Chumba kilikuwa kidogo, kimechoka, na dirisha lake lilikuwa linaangalia ukuta wa jengo lingine. Lakini kwa Muga, hicho kilikuwa mwanzo mpya.

Usiku wa Valentine, mitaa ilikuwa imejaa mapenzi. Couples wanacheka, wanapiga selfie, wanakula pamoja. Muga alikaa kitandani, akaangalia simu, akafungua WhatsApp, hakuna hata “Happy Valentine”.

Akatabasamu kidogo, akajisemea:
“Labda zamu yangu bado haijafika.”

Maoni

Machapisho Maarufu